Sunday, May 5, 2013

HABARI NA PICHA KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA JIJINI ARUSHA KATIKA UFUNGUZI WA PAROKIA MPYA YA KANISA KATOLIKI OLASITI


 Majeruhi wa mlipuko akipatiwa huduma ya kwanza

Majeruhi wakiwa katika hali mbaya


IMEELEZWA KUWA MCHANA WA LEO MAJIRA YA SAA SABA, JIJINI ARUSHA UMETOKEA MLIPUKO MKUBWA WA KITU KINACHODHANIA KUWA NI BOMU. 
MLIPUKO HUO UMETOKEA KATIKA KANISA KATOLIKI PAROKIA MPYA YA OLASITI, ILIYOKUWA KATIKA HARAKATI NA SHAMBRA SHAMBRA ZA KUZINDULIWA RASMI LEO JIJINI HUMO. 
MLIPUKO HUO UMETOKEA WAKATI WAUMINI WA KANISA HILO LA KATOLIKI WAKIENDELEA NA SHEREHE ZA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA.
AIDHA IMEELEZWA NA MASHUHUDA KWA NJIA YA SIMU KATIKA MTANDAO HUU KUWA KUWA KUNA WATU KADHAA WAMEPOTEZA MAISHA NA WENGINE WENGI KUJERUHIWA AMBAO WENGI WAO WALIKIMBIZWA HOSPITALI.

 Polisi wakiendelea kufanya uchunguzi
 Eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa ni bomu lilipotua na kulipuka katika kanisa


No comments:

Post a Comment