Friday, September 21, 2012

MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA UWEPO WA RPC WA IRINGA KAMUHANDA YAPIGWA STOP

 Polisi wakiwa tayari kuhakikisha hakuna kufanyika kwa maandamano

 Mh. Peter Msigwa akiongea na wananchi na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa maandamano hayo

 Mh. Peter Msigwa mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)


 
Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Msigwa, akizungumza na wanachama na wapenzi wa chama hicho katika ofisi za Wilaya za chama hicho kuhusu kuahirishwa kwa maandamano ya amani  yaliyokuwa yafanyike siku ya leo kushinikiza kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kujiuzulu kutokana na kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten Daudi mwangosi kilichotokea tarehe 2 septemba mwaka huu. 
 
Msigwa amesema kutokana na barua aliyoipata toka kwa zikitaka kusitisha maandamano hayo, aneleza barua inawataka kusitisha na kueleza kuwa sababu kubwa ni kwamba maandamano hayo hayataweza kuwa na polisi wa kusimamia na kukataza kufikia katika ofisi ya RPC  ambayo ni ofisi ya kiserikali.
 
Hata hivyo Msigwa ameeleza kuwa msimamo wao uko pale pale ila anajiandaa kujibu hoja za barua hiyo na kuwataka wananchi wawe na subira mpaka atakapowatangazia tena kuwepo kwa maandamano hayo ya amani.
 
Wakati huo huo wameonekana askari wakiwa katika magari yao kudhibiti wananchi kuandamana. Hali hiyo ilitokana na wananchi  hao kumiminika kwenye ofisi za Chadema mjini hapa kwa ajili ya kujiandaa maandamano. (Chanzo: Msigwablog)

Monday, September 10, 2012

Ommy Dimpoz-Baadae (Official Video)