Polisi wakiwa tayari kuhakikisha hakuna kufanyika kwa maandamano
Mh. Peter Msigwa akiongea na wananchi na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa maandamano hayo
Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Peter Msigwa, akizungumza na wanachama na wapenzi wa
chama hicho katika ofisi za Wilaya za chama hicho kuhusu kuahirishwa kwa
maandamano ya amani yaliyokuwa yafanyike
siku ya leo kushinikiza kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kujiuzulu
kutokana na kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten Daudi mwangosi
kilichotokea tarehe 2 septemba mwaka huu.
Msigwa amesema kutokana na barua aliyoipata toka kwa zikitaka
kusitisha maandamano hayo, aneleza barua inawataka kusitisha na kueleza kuwa
sababu kubwa ni kwamba maandamano hayo hayataweza kuwa na polisi wa kusimamia
na kukataza kufikia katika ofisi ya RPC
ambayo ni ofisi ya kiserikali.
Hata hivyo Msigwa ameeleza kuwa msimamo wao uko pale pale ila
anajiandaa kujibu hoja za barua hiyo na kuwataka wananchi wawe na subira mpaka
atakapowatangazia tena kuwepo kwa maandamano hayo ya amani.
Wakati huo huo wameonekana askari wakiwa katika magari yao
kudhibiti wananchi kuandamana. Hali hiyo ilitokana na wananchi hao kumiminika kwenye ofisi za Chadema mjini
hapa kwa ajili ya kujiandaa maandamano. (Chanzo: Msigwablog)
|
No comments:
Post a Comment